Tigo yazindua ‘Tigo Internet Mega Boksi‘

Tigo introduces new internet service: ‘Tigo Internet Mega Boksi‘
 
 
Spread the Word
Listed Under

Tags:
* Tigo
* Internet
* Mega Boksi

Industry:
* Telecom

Location:
* Tanzania

Subject:
* Services

June 7, 2012 - PRLog -- Matumizi ya mtandao yamebadili dunia ambayo tunaishi na na kubadili jinsi ya kujua ukweli. Kama kampuni inayojali watumiaji wake, Tigo ilianzisha huduma na bidhaa za mtandao mwaka 2011 na imeendelea kuzingatia mahitaji ya wateja wake. Kwa kuzingatia hilo, Tigo imeanzisha huduma mpya za mtandao: ‘Tigo Internet Mega Boksi,’ kusaidia wateja kuwa karibu na habari za ulimwengu katika ulimwengu huu wenye teknolojia ya hali ya juu.

Vifurushi hivi vipya vya mtandao vitawawezesha wateja kununua vifurushi vinachoendana na mahitaji yao. Mteja anaweza kununua kifurushi cha siku, wiki au mwezi, pamoja na kufanya uteuzi unaoendana na matumizi ya huduma mbalimbali za kimtandao  kuendana na matumizi yake. Vifurushi vyote vinajumuisha matumizi ya barua pepe, Facebook, Twitter na kuvinjari kwenye mtandao bure. Vifurushi vyote ni vya kasi isiyo na ukomo.

“Tumesikiliza mahitaji ya wateja wetu na kutathmini mahitaji yao. Tumewaletea vifurushi hivi rahisi ili kuwezesha huduma zinazotumiwa na wateja wengi kuwa bure na zisizo na kikomo” alisema Alice Maro, afisa Uhusiano wa Tigo.

Jinsi ya Kujiunga:

Kwa kupiga *148*01#  wateja  watapata fursa ya kuchagua muda wa vifurushi wanavyohitaji, inaweza kuwa kwa siku, wiki au mwezi kutegemeana na matumizi yao. Watumiaji wa modem za Tigo wanaweza kununua vifurushi hivi kwa kutumia  programu mbalimbali zinazopatikana kwenye modem za Tigo. Bei zinaanzia sh. 450 kwa kifurushi cha siku.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi wa kwanza Tanzania, ulianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini unaotoa huduma katika mikoa 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 43 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo  • Simu 255 713 123754
End
Email:***@trinitypromotions.co.tz Email Verified
Account Email Address Verified     Account Phone Number Verified     Disclaimer     Report Abuse
Trinity Promotions Ltd. News
Trending
Most Viewed
Daily NewsLike PRLog?
9K2K1K
Click to Share